
Beki wa kati wa klabu ya Yanga na Taifa Stars, Kelvin Yondani. ameondolewa
kwenye kikosi cha timu ya taifa kufuatia kupatwa na majeraha ya mguu.Yondani sasa ataukosa mchezo ambao Stars ambayo itacheza dhidi ya Uganda Septemba 8 wiki hii kwenye Uwanja wa Nambole huko Kampala.
Mchezaji huyo ameumia mguu na kwa mujibu wa daktari wa timu ameshauri ni vema akasalia nchini kwa ajili ya matibabu zaidi.
Wakati huo kikosi cha Stars kinaondoka leo nchini kuelekea huko Kampala tayari kukipiga na Uganda kwenye kipute cha kufuzu kuelekea AFCON 2019.
No comments:
Post a Comment