Tuesday, 4 September 2018

NGOMA ATUMA SALAMU LIGI KUU TANZANIA BARA

NGOMA ATUMA SALAMU!!!
Mshambuliaji wa Azam FC, Donald Ngoma, ameanza rasmi mazoezi ya kuchezea mpira na wenzake.
Ngoma aliyekuwa akifanya mazoezi mepesi kwa kipindi chote kwa takribani wiki sita, amepona majeraha ya kuchanika mtulinga wa kati wa goti lake la mguu wa kulia yaliyokuwa yakimsumbua.
Nyota huyo kutoka Zimbabwe alianza na mazoezi ya viungo ya kawaida kabla ya kuhamia kwenye yale ya kuchezea mpira, jana ambapo anatarajia kuendelea na programu hiyo hadi atakapokuwa fiti kabisa kwa asilimia 100

No comments: