Tuesday, 4 September 2018

SAMATTA ULIMWENGU WAWASILI KAMBI YA STARS

Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta ameshawasili nchini na kujiunga na kambi ya timu ya taifa.
Samatta ambaye anaicheza Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji aliwasili akiwa pamoja na mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan, Thomas Ulimwengu, alfajiri ya leo Jumanne kisha moja kwa moja wakaeleka kujiunga na kambi ya timu ya Taifa
Taifa Stars inajiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) dhidi ya Uganda

No comments: